Dodoma. Bunge limeelezwa zaidi
ya Dola za Marekani 1.25 bilioni
sawa na Sh2 trilioni hutoroshwa
na kupelekwa nje ya nchi kila
mwaka kwa lengo la kukwepa
kodi.
Taarifa hiyo imetolewa wakati
wingu zito likiwa limegubika
uwasilishaji wa ripoti ya kikosi
kazi cha Serikali
kilichochunguza sakata la Sh315
bilioni zilizofichwa na
Watanzania katika mabenki
nchini Uswisi.
Takwimu hizo zilitolewa juzi na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Zitto alisema taarifa mbalimbali
zinaonyesha kuwa Tanzania
inapoteza kila mwaka mapato
hayo ambayo ni sawa na
asilimia tano ya Pato la Taifa
kupitia uhamishaji huo haramu.
“Uhamishaji huu haramu wa
fedha kupelekwa nje ya nchi
hufanywa kwa lengo la kukwepa
kulipa kodi au wahusika
kuepuka kukamatwa na fedha
walizopata kwa kupokea
rushwa,” alisema Zitto.
Kamati hiyo imependekeza
Bunge kutunga sheria
itakayodhibiti uhamishaji
haramu au ufichaji wa fedha nje
ya kwa lengo la kuogopa
kukamatwa na rushwa, kufanya
ufisadi na kukwepa kodi.
Zitto alisema hayo ni moja ya
maazimio yaliyofikiwa katika
mkutano wa 10 wa Jumuiya ya
Kamati za Hesabu za Serikali za
Mabunge (Sadcopac) ya Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(Sadc).
Alisema katika mkutano huo
uliofanyika Septemba 2 hadi 7,
mwaka huu Jijini Arusha,
wajumbe waliazimia
kuhamasisha mabunge ya nchi
zao kutunga sheria kudhibiti
uhamishaji huo wa fedha.
Wiki iliyopita, mbunge wa
Kisesa, Luhaga Mpina (CCM),
alikaririwa akisema bungeni
‘hapatatosha’ kama ripoti ya
mabilioni ya Uswisi
haitawasilishwa katika Bunge
hili.
Mpina alisema yeye ni miongoni
mwa wabunge waliohojiwa
baada ya kutamka bungeni kuwa
zaidi ya Sh11.9 trilioni
zimetoroshwa kutoka Tanzania
kati ya mwaka 1970 na mwaka
2008.
“Nilipolisema hilo jambo
niliikabidhi Serikali kupitia
Bunge taarifa za tafiti
mbalimbali ili ifuatilie. Baadaye
Zitto akaja na hoja ya bilioni
314… tunataka taarifa
hatutanii,” alisema.
Ripoti hiyo ilikuwa iwasilishwe
Bunge la Aprili lakini Serikali
ikaomba muda zaidi na kuahidi
kuiwasilisha katika Mkutano wa
14 wa Bunge unaoendelea Mjini
Dodoma.
chanzo""""mwananchi
posted by kulwa ngatigwa
No comments:
Post a Comment