Monday, 9 December 2013

Kenya yaanza njama kwa Kili Stars

Uganda imeliachia Kombe la Chalenji baada ya kuchapwa kwa penalti 3-2 na Kilimanjaro Stars kwenye Uwanja wa Manispaa ya Mombasa.

Mombasa.Wenyeji Kenya
wameingia mchecheto na makali
ya Kilimanjaro Stars baada ya
kulazimisha mchezo wa nusu
fainali ufanyike Machakos
badala ya Mombasa.
Awali nusu fainali hiyo ilikuwa
ichezwe Mombasa, lakini
kutokana na hali ya joto ambayo
inaibeba Tanzania kulinganisha
na Kenya ambayo wachezaji
wake wengi wanaishi Nairobi
kwenye baridi.
Baada ya mechi dhidi ya
Rwanda, ambapo Kenya
ilishinda bao 1-0, Kocha Adel
Amrouche alikiri kwamba; “Hali
ya hewa ya Mombasa si nzuri
kwetu ni joto kiasi na wachezaji
wangu hawajazoea.”
Habari za ndani zinadai baada
ya Uwanja wa Kisumu
kushindikana kumalizika kwa
wakati waandaji walipanga
mechi za nusu fainali zichezwe
Mombasa na fainali ikachezwe
Nyayo mjini Nairobi, lakini kwa
hali waliyoiona katika mechi za
juzi Jumamosi wenyeji
wakaamua kupeleka mechi ya
Kili Stars dhidi ya Kenya huko
Machakos. Mechi nyingine ya
nusu fainali itachezwa mjini
Mombasa.
Habari za ndani zinadai kwamba
Adel amewaambia viongozi wake
kwamba endapo Kenya ikicheza
na Stars mjini Mombasa itakuwa
kwenye wakati mgumu kutokana
na Tanzania kuzoea hali ya joto
na vilevile ina sapoti kubwa
Mombasa kwa vile ni jirani na
Tanga.
Kenya iko kwenye presha ya
kufuzu fainali kwani siku ya
fainali nchi hiyo itakuwa
ikisherehekea miaka 50 ya
uhuru wake.
UGANDA WAUTEMA UBINGWA
Uganda imeliachia Kombe la
Chalenji baada ya kuchapwa kwa
penalti 3-2 na Kilimanjaro Stars
kwenye Uwanja wa Manispaa ya
Mombasa.
Kocha wa Uganda, Sredejovic
Milutin ‘Micho’ na wachezaji
wake waliingia kwenye mchezo
huo kwa kujiamini, ambapo
walicheza kwa kutulia na
kushambulia kwa kumtumia
winga Dan Sserunkuma
aliyetumia dakika 16 tu kufunga
bao la kuongoza kabla ya Mrisho
Ngassa kusawazisha dakika mbili
baadaye na akafunga tena la pili
dakika ya 38.
Beki mrefu wa Uganda, Martin
Mpunga alifunga bao la pili la
Uganda dakika ya 73 na
kusababisha timu hizo kwenda
kwenye penalti kwani dakika 90
zilimalizika kwa sare ya mabao
2-2.
Stars ilianza kuwachanganya
Uganda mapema baada ya
kusawazisha bao lao na
kuwaongeza jingine na
kuwalazimisha kwenda kipindi
cha kwanza wakiwa nyuma kwa
mabao 2-1.
Hali hiyo ilizua utata kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo
kwani kocha Micho alisikika
akiwafokea wachezaji wake na
kuwaambia waache upuuzi kwa
vile wamebeba hadhi ya
mamilioni ya raia wa Uganda.
chanzo-mwananchi


posted by kulwa ngatigwa

No comments:

Post a Comment