Tuesday, 17 December 2013

Chelsea watibuliwa na Sunderland

*Watupwa nje ya Kombe la Ligi
*Man City waingia nusu fainali


Mawazo ya ‘kawaida’ ya Chelsea
kuingia nusu fainali ya Kombe la
Ligi yaligeuka ndoto ya mchana
baada ya kutibuliwa na Sunderland.
Wakiongoza kwa bao 1-0 hadi
kuelekea mwisho wa mchezo,
Chelsea walijikuta wakiadabishwa
na mchezaji wao wa zamani, Fabio
Borini aliyeingia kipindi cha pili na
kutikisa nyavu zao.
Bao la Chelsea lilifungwa mara tu
baada ya kuanza kipindi cha pili na
Frank Lampard, ambapo kwa mara
ya kwanza kwenye michuano hii
teknolojia ya goli ilitumika.
Lampard anatambulika kwa bao
lake kwa England dhidi ya
Ujerumani kukataliwa kutokana na
macho ya mwanadamu kushindwa
kuona vyema.
Lakini usiku wa Jumanne hii
mwamuzi hakuwa na tabu, bali
kifaa alichovaa mkononi
kilimwonesha kwamba ni bao, licha
ya kipa Tito Mannone kuuvuta
mpira haraka kutoka nyuma ya
mstari.
Wakati timu zikielekea kukamilisha
kipindi cha pili huku kocha wa
Chelsea, Jose Mourinho akijidai kwa
kutembea tembea eneo lake la
kujidai, Borini aliwaadhiri dakika ya
88
Walipoingia katika muda wa zaida,
walitoshana nguvu huku kila
upande ukikosa mabao na alikuwa
mchezaji wa Korea, Ki Sung-Yueng
aliyewatesa mabeki, akageuka na
kuweka mpira kimiani dakika ya
118.
MANCHESTER CITY NUSU FAINALI
Manchester City wameingia nusu
fainali ya Kombe la Ligi msimu huu.
Man City wanaofundishwa na
Manuel Pellegrini walivuka baada
ya kupata ushindi wa mabao 3-1
dhidi ya vijana wa Leicester City
wanaocheza kwenye Championship.
Man City wanaojulikana zaidi siku
hizi kwa mtindo wao wa kuachia
mvua ya mabao wakiwa nyumbani,
lakini jioni ya Jumanne hii walikuwa
ugenini.
Kwa hiyo matatu kutoka kwa
Aleksandar Kolarov na Edin Dzeko
aliyefunga mawili, yaliwatosha
wakati wenyeji walipata bao la
kufutia machozi kutoka kwa Lloyd
Dyer.
Jumatano hii katika robo fainali
nyingine, Stoke watakuwa wenyeji
wa Manchester United wakati
Tottenham Hotspur waliomfukuza
kocha wao, Andre Villas-Boas
watakabiliana na West Ham kwenye
dimba lile lile ambalo Liverpool
waliwanyoa 5-0 Jumapili hii.


posted by kulwa ngatigwa

No comments:

Post a Comment