Timu hiyo ya Kilimanjaro Stars
itacheza saa 7:30 mchana kwenye
uwanja huo ambao katika mchezo
wa kwanza ilicheza hapo na kutoka
sare ya bao 1-1 na Zambia, ambayo
itacheza na Sudan nusu fainali ya
pili mjini Mombasa.
Katika uwanja ambao Stars
itachezea kuna huduma za kifahari
vyumbani kama runinga za kisasa
zilizounganishwa na digitali,
vinywaji laini vya kila aina, chai na
maji ya moto ya kuoga jambo
ambalo linaufanya uwe tofauti na
viwanja vingine vya Afrika
Mashariki na Kati ingawa bado
nyasi haziridhishi hasa mvua
inaponyesha.
Kocha wa Stars, Kim Poulsen
amesisitiza kwamba katika mchezo
huo watashambulia kama
walivyofanya dhidi ya Uganda mjini
Mombasa mwishoni mwa wiki.
Kim alisema: “Ni mchezo mgumu
sana ulioko mbele yetu lakini
naamini kwamba tupo tayari
kushinda katika mazingira yoyote
yale, nina kikosi imara ambacho
kimeimarika kimchezo, nina imani
tutavuka.”
“Hakutakuwa na mabadiliko
makubwa sana kikosini kwa vile
tuna wachezaji wengi ambao wako
tayari kwa mchezo,lengo sasa ni
kucheza fainali na ninaamini huo
uwezo upo tuna mastraika wazuri,
mabeki na viungo.
“Tutacheza mchezo kwa staili
tofauti zaidi, tunajua Kenya itakuwa
na faida ya uenyeji kuanzia
mashabiki na kila kitu lakini
haitatusumbua, tutafanya kazi yetu
uwanjani,”alisisitiza Poulsen
ambaye asilimia kubwa ya kikosi
chake wachezaji wake wamefanya
vizuri kwenye ligi zao.
Habari za ndani zinadai kwamba
Kenya ilifanya mpango wa
kuhamisha mchezo huo kutoka
Mombasa hadi Machakos kutokana
na hali ya hewa.
Mombasa ni joto, hali ambayo
Tanzania wameizoea lakini Kenya
inawapa taabu kutokana na
wachezaji wake kuzoea baridi ya
jijini Nairobi. Kocha Adel Amrouche
alisema; “Tanzania ni ngumu ina
mastraika wazuri, tunajua inaingia
ikiwa na morali ya kumtoa bingwa
mtetezi, lakini sisi tutacheza soka
yetu na ninaamini Kenya kiufundi
ipo sawa tayari kwa fainali za
Alhamisi.”
Kenya itakuwa ikiwategemea
mastraika wake Allan Wanga na
Jacob Kelli huku Stars ikiwa na
ukuta imara wa Kelvin Yondani na
Said Morad huku langoni akizuia
Ivo Mapunda.
Kiungo cha Stars huenda
akasimama Athuman Iddi ‘Chuji’ na
Frank Domayo ambao watakuwa
wakitengeneza mipira kwa
wachezaji wa pembeni Amri Kiemba
na Mrisho Ngassa.
Stars imeonyesha mabadiliko
makubwa kiuchezaji haswa baada
ya kuingia kwa Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu ambao
wameonyesha kujiamini na
wanacheza soka la kufundishwa
jambo ambalo limewafanya wawe
gumzo zaidi.
chanzo. mwanaspoti
posted by kulwa ngatigwa
No comments:
Post a Comment