Monday, 9 December 2013

MAAJABU 10 MSIBA WA MANDELA

Kifo chake kimeushtua
ulimwengu na kwa mara ya
kwanza katika historia, dunia
nzima imesimama nyuma ya
jemedari huyo , kila mmoja
akionesha masikitiko yake .
Wakati dunia ikisubiri mazishi
yake ambayo pia yatavunja
rekodi ya mazishi yote
yaliyowahi kufanywa tokea
kuumbwa kwa uso wa dunia
hapo Desemba 15 mwaka huu,
Uwazi limebaini maajabu kumi
yanayoambatana na msiba
huo.
AIR FORCE ONE KUBEBA
MARAIS WATANO WA
MAREKANI
AIR Force One ni ndege
inayombeba Rais wa Marekani
aliye madarakani na
kumpeleka popote duniani .
Lakini katika hali ya
kushangaza, Idara ya Usalama
ya Marekani imetoa ruhusa
kwa marais wastaafu wakiwa
na wake zao , kuandamana na
Rais Barak Obama kuhudhuria
mazishi ya shujaa huyo wa
dunia.
Hii ni mara ya kwanza katika
historia ya taifa hilo lenye
nguvu kubwa duniani
kuwapakia katika ndege hiyo
yenye kila kitu ndani yake,
marais wake kwa wakati
mmoja .
Marais hao ni Obama
mwenyewe na mkewe
Michelle, George Bush na
mkewe Laura, Bill Clinton na
mkewe Hillary , Rais wa 39 wa
Marekani, Jimmy Carter naye
atakuwepo ila baba yake
George W. Bush , George Bush
senior huenda asiende
kutokana na urefu wa safari
hiyo.
QUNU; KIJIJI
KITAKACHOLNDWA KULIKO
VYOTE DUNIANI
Mandela alizaliwa katika Kijiji
cha Qunu, kilichopo katika
Jimbo la Eastern Cape ,
kilometa 32 Kusini Magharibi
mwa mji wa Mthatha .
Kutokana na tukio hilo kubwa
la mazishi, Jeshi la Afrika
Kusini ambalo ni bora zaidi
barani Afrika, limechukua
jukumu la kusimamia ulinzi
wote. Lakini uwepo wa Rais
Obama na watangulizi wake
wanne, utaifanya nchi hiyo
kuchukua tahadhari zaidi ya
kuhakikisha hakuna dosari
yoyote ya kiusalama
inayoweza kujitokeza .
Ulinzi huo umeimarishwa zaidi
kutokana na ukweli kwamba
viongozi wakubwa karibu wote
wa dunia watahudhuria
mazishi hayo , akiwemo Papa
Francisco, Waziri Mkuu wa
Uingereza, David Cameron na
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon. Hakuna
uwezekano wowote wa Al
shaabab kusababisha rabsha
kwani wameshadhibitiwa kwa
ulinzi mkali.
MANDELA ALIKUWA ‘GAIDI ’
PEKEE ALIYEGEUKA KUWA
SHUJAA
Kwa miaka mingi, mataifa ya
magharibi pamoja na Marekani
walimchukulia Mandela na
harakati zake kama gaidi .
Wakati wa utawala wa ubaguzi
wa rangi nchini Afrika Kusini,
chama cha ANC kilikuwa na
jeshi lake lililofahamika kama
Umkhonto we Sizwe. Wazungu
wa Magharibi na Marekani
ambao walikuwa wakiwaunga
mkono Makaburu , waliiona
ANC kama kikundi cha kigaidi
na hivyo Mandela naye
akawekwa katika orodha ya
magaidi duniani .
Hata hivyo, baada ya kutoka
jela na kuchaguliwa kuwa Rais
wa Afrika Kusini , Mandela
aligeuka kuwa kipenzi cha
watu hao ambao walilazimika
kumuondoa katika orodha ya
magaidi na leo hii akiwa
amefariki dunia , anapewa
heshima kubwa kuliko
aliyowahi kupewa mzungu
yeyote duniani.
MWEUSI PEKEE
ALIYENYENYEKEWA NA
WAZUNGU
Hayati Mandela ndiye mtu
mweusi pekee duniani
aliyewahi kupewa heshima
zisizo na mfano tokea
kuumbwa kwa dunia. Mara
baada ya kutangazwa kwa kifo
chake, viongozi wa mataifa
yote makubwa duniani
walionesha masikitiko yao na
kila mmoja alimsifu kama mtu
wa aina ya pekee kuwahi
kuwepo chini ya jua (ukiachia
mbali mitume na manabii) .
JENGO LA SERIKALI NEW
YORK LAPAKWA RANGI YA
BENDERA YA SAUZI
Jengo moja la serikali jijini
New York , Marekani
limebadilishwa taa za
kulipamba na kuonesha
bendera ya taifa la Afrika
Kusini.
WENYEJI WAHAMA , WAGENI
WAMILIKI NYUMBA QUNU
Kijiji cha Qunu, sehemu
ambayo yatafanyika mazishi ya
Mandela, kuna eneo dogo
kulingana na ugeni mkubwa
unaotarajiwa kuwepo . Taarifa
kutoka huko zinasema wenyeji,
pamoja na machungu
waliyonayo kutokana na kifo
cha mzee huyo , pia
watafaidika kiuchumi kutokana
na wageni wengi kutaka
kupata nyumba za kukaa
wakati wakiendelea na
maombolezo.
Wanaotafuta nyumba kijijini
hapo ni pamoja na watu
kutoka vyombo mbalimbali
vya habari , mashirika ya
kimataifa na wageni binafsi .
Inadaiwa kuwa wenyeji
wanasogea katika vijiji vya
jirani ili kupangisha nyumba
zao kwa muda.
MECHI ZA LIGI KUU
ENGLAND ZAANZA KWA
SALA
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida, Chama cha Soka cha
England ( FA) kiliamuru mechi
zote za ligi kuu zilizochezwa
wiki iliyopita , lazima zianze
kwa sala maalum ya kumuenzi
mzee Mandela .
Hii ni mara ya kwanza kwa
agizo hilo kutolewa kwa
heshima ya kiongozi mstaafu
aliyefariki dunia asiye
Mwingereza, tena akitokea
barani Afrika. Tukio kama hilo
pia limefanywa na Shirikisho
la Soka la Kimataifa ( FIFA)
ambalo limeamuru bendera
yake iliyo katika mataifa yote
wanachama duniani, ishushwe
nusu mlingoti kwa heshima ya
Tata Madiba !
NASA YATOA ZAWADI YA
PICHA YA SAUZI KUTOKA
ANGANI
Taasisi ya utafiti wa anga za
juu nchini Marekani (NASA)
kwa kutambua mchango
mkubwa wa Mandela katika
amani ya dunia, imetangaza
kutoa zawadi kwa watu wa
Afrika Kusini , itakayoonesha
picha ya nchi hiyo
inavyoonekana kutoka angani .
UINGEREZA YAAGIZA BALOZI
ZOTE KUSHUSHA NUSU
MLINGOTI
Serikali ya Uingereza
imeziagiza balozi zote za kigeni
zilizopo nchini humo kushusha
bendera zao nusu mlingoti
kama moja ya heshima na
maombolezo ya kifo cha Mzee
Nelson Mandela .
Hili ni agizo la aina yake
kuwahi kutolewa kuhusiana na
msiba wa kiongozi yeyote,
kwani suala la kushusha
bendera mara nyingi ni
uamuzi wa serikali husika na si
kwa shinikizo kama ilivyotokea
Uingereza.
AMSAFIRISHA PAPA
MAZISHINI
Historia ya utumishi wa
kiongozi mkuu wa Madhehebu
ya Romani , papa haioneshi
kama aliwahi kuhudhuria
mazishi ya rais au rais
mstaafu, kitendo cha Papa
Francisco kuhudhuria mazishi
hayo kumeongeza ajabu katika
mazishi ya Mandela , wengi
wakisema hakina hakuwa mtu
wa kawaida.

No comments:

Post a Comment