Saturday, 21 December 2013

WATANI KUAMUA NANI JEMBE TAIFA LEO

Mashabiki wa timu ya Yanga Fc.
Mashabiki wa timu ya Simba Fc.

WATANI wa jadi katika soka
nchini, timu za Yanga na Simba,
leo zinashuka katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam
kuhitimisha majigambo ya ‘Nani
Mtani Jembe’ baina yao katika
mechi kali inayofanyika chini ya
uratibu wa mdhamini wao,
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Mbali ya wapenzi na mashabiki wa
timu hizo kusubiri kuona ‘nani
mtani jembe’ kati yao, pia
watapata fursa ya kushuhudia
nyota wapya waliosajiliwa kupitia
dirisha dogo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
jana, Kaimu Katibu Mkuu na Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Boniface
Wambura, alisema maandalizi ya
mechi hiyo ya aina yake
yamekamilika.
Wambura alisema vikosi vya ulinzi
na usalama katika mechi ya leo
vimekamilika kila idara na
kwamba Barabara ya Taifa
inayoanzia Keko-Maghorofani hadi
Barabara ya Mandela, itafungwa
kuanzia saa 12 asubuhi kupisha
hekaheka za mtifuano huo.
Alisema magari hayataruhusiwa
kuegeshwa kuanzia eneo la Baa ya
Minazini hadi msikiti
unaotazamana na Uwanja wa
Uhuru, hivyo magari yote
yataegeshwa nje ya Uwanja wa
Ndani wa Taifa – kando ya
Barabara ya Mandela.
“Magari yatakayoruhusiwa kuingia
maeneo hayo na hata ndani ya
Uwanja wa Taifa ni yatakayokuwa
na stika zilizotolewa na TFF.
Tunawaomba wadau na mashabiki
wa soka kuheshimu na kutii
maagizo ya vikosi vya ulinzi,”
alisema Wambura.
Aliongeza kuwa milango ya
kuingilia uwanjani itakuwa wazi
kuanzia saa sita mchana ambapo
baada ya mauzo ya tiketi ya jana,
zoezi hilo litaendelea leo nje ya
uwanja huo kabla ya mechi ili
kuwapa mashabiki fursa ya kukata
na kuingia moja kwa moja.
Pambano la leo linasubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa soka
wanaohitaji sio tu kuona nyota
wapya waliosajiliwa na klabu hizo,
pia kujua ‘nani jembe’ ndani ya
uwanja kwani kwa nje ya uwanja,
Yanga ni kama imeshinda
kutokana na kuwa kwenye
mazingira mazuri kisaikolojia.
Nje ya uwanja, Nani Mtani Jembe
ilihusisha vita baina ya mashabiki
wa kila klabu ‘kupora’ mamilioni
ya mwingine kupitia shindano la
kinywaji cha Kilimanjaro Premium
Lager ambapo Simba ilizidiwa na
Yanga kwa kiasi kikubwa cha pesa.
Ukiondoa shangwe ya mashabiki
wa Yanga kumpata mshambuliaji
wa kimataifa wa Uganda,
Emmanuel Okwi akitokea SC Villa
ya Uganda na Juma Kaseja, Simba
leo itakuwa na makipa waliowahi
kudaka Jangwani kwa vipindi
tofauti, Ivo Mapunda na Yaw
Berko.
Nyuma ya majina hayo makubwa,
Yanga ilinasa saini ya kiungo
Hassan Dilunga kutoka Ruvu
Shooting ya Pwani, wakati Simba
iliwasainisha kwa mpigo kiungo
mchezeshaji Awadh Juma Issa
kutoka Mtibwa Sugar ya
Morogoro na Ally Badru Ally
kutoka Canal Suez ya Misri.
Kila timu ilishajichimbia kambini
kunoa makucha kuelekea
pambano hilo ili kusawazisha
makosa yaliyowafanya watani hao
kutoka sare ya 3-3 katika mechi
ya raundi ya kwanza ya Ligi Kuu
Bara iliyochezwa Oktoba 20.
Uwepo wa nyota wapya kwa kila
upande ambao watashirikiana na
wakali wengine, unalifanya
pambano la leo liwe lenye mvuto
wa aina yake ambapo kiingilio cha
chini ni sh 5,000 kwa viti vya
kijani.
Kwa upande wa viti vya rangi ya
bluu, kiingilio ni sh 7,000; viti
vya rangi ya chungwa sh 10,000;
VIP C ni sh 15,000; VIP B sh
20,000 huku VIP A sh 40,000.
Kwa upande wa waamuzi, kati
atasimama Ramadhan Ibada ‘Kibo’
wa Zanzibar, atakayesaidiwa na
Ferdinand Chacha wa Bukoba na
Simon Charles wa Dodoma huku
Israel Nkongo wa Dar es Salaam
akiwa mezani. Kazi ya kutathimini
utendaji wa waamuzi wote
itakuwa chini ya Soud Abdi wa
Arusha.
MECHI TANGU 2010
Rekodi ya watani hawa
inaonyesha kuwa mechi ya leo ni
ya tisa tangu mwaka 2010 na
katika mechi nane, Yanga
imeshinda tatu, Simba mbili na
wamekwenda sare tatu.
Aprili 18, 2010: Simba 4, Yanga 3
Oktoba 16, 2010: Yanga 1, Simba
0
Machi 5, 2011: Yanga 1, Simba 1
Oktoba 29, 2011: Yanga 1, Simba
0
Mei 6, 2012: Simba 5, Yanga 0
Oktoba 3, 2012: Yanga 1, Simba 1
Mei 18, 2013: Yanga 2, Simba 0
Oktoba 20, 2013: Simba 3, Yanga
3


posted by kulwa ngatigwa

Tuesday, 17 December 2013

KIUNO BILA MFUPA

hatari sana

posted by kulwa ngatigwa

Hili ndio gari jingine jipya la Jaguar wa Kenya

JAGUAR
Gari la jaguar

Mwanamuziki maarufu toka 254
Jaguar alionekana akiendesha
Gari lake jipya  aina ya Jaguar
kama lilivo jina lake wikiendi
iliyopita kwenye concert
lililoandaliwa na kampuni moja
ya simu kwenye uwanja wa
Kasakani.
Mwimbaji huyo anaefahamika
sana kwa magari ya bei mbaya
anayoendesha aliwashangaza
maelfu ya watu waliokazana
kwenye tamasha hilo walati
alipoitwa jukwaani ambapo
alishuka toka kwenye gari hilo
na kupanda jukwaani mara moja.
Jaguar huyuhuyu mapema
mwaka huu 2013 aliripotiwa
kununua ndege binafsi.


posted by kulwa ngatigwa

MBUNGE AMPONDA MISS TANZANIA KWA KUTOKUJUA KUONGEA KISWAHILI

Miss Tanzania 2012, Brigitte
Alfred hajui Kiswahili? Well,
tuliowahi kukaa naye kidogo
tunaweza kumtetea kuwa anakijua
haswaa, sema hupendelea zaidi
kuongea kimombo. Pengine ndio
maana mbunge wa viti maalum
kutoka Zanzibar, Rukia Ahmed
anahisi mrembo huyo haijui lugha
yake ya taifa.
Akiongea bungeni leo, Bi. Rukia
amesema Brigitte Alfred hafai
kuiwakilisha Tanzania kwakuwa
hawezi kuzungumza Kiswahili.
Mbunge huyo alienda mbali zaidi
kwa kupendekeza mashindano ya
Miss Tanzania yafutwe na badala
yake yawekwe mashindano ya
Sayansi kwa manufaa ya taifa.
Akijibu kauli hiyo, Brigitte
amesema: Meanwhile as our
county suffers from 3rd world
problems this is what is being
discussed bungeni. I would love
to meet this this woman! Asante
mama,” ameandika mrembo huyo
kwenye Instagram. “All of your
comments give me hope that
there’s still sensibility out here,”
aliongeza.
“Mh.Rukia amekosa mada
bungeni?
*rollingmyeyesoutloud*,”
alitweet.
“Anko in the office must be
jumping for joy right now-they
love to say ‘I told you so’-In
Kiswahili ofcourse.”
Hata hivyo Waziri wa Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo
Dkt Fenella Mukangara alisema
serikali haiwezi kuyafuta
mashindano hayo kwakuwa yana
umuhimu mkubwa kwa taifa na
yamekuwa yakiitangaza nchi na
shughuli za utalii.


posted by kulwa ngatigwa

Chelsea watibuliwa na Sunderland

*Watupwa nje ya Kombe la Ligi
*Man City waingia nusu fainali


Mawazo ya ‘kawaida’ ya Chelsea
kuingia nusu fainali ya Kombe la
Ligi yaligeuka ndoto ya mchana
baada ya kutibuliwa na Sunderland.
Wakiongoza kwa bao 1-0 hadi
kuelekea mwisho wa mchezo,
Chelsea walijikuta wakiadabishwa
na mchezaji wao wa zamani, Fabio
Borini aliyeingia kipindi cha pili na
kutikisa nyavu zao.
Bao la Chelsea lilifungwa mara tu
baada ya kuanza kipindi cha pili na
Frank Lampard, ambapo kwa mara
ya kwanza kwenye michuano hii
teknolojia ya goli ilitumika.
Lampard anatambulika kwa bao
lake kwa England dhidi ya
Ujerumani kukataliwa kutokana na
macho ya mwanadamu kushindwa
kuona vyema.
Lakini usiku wa Jumanne hii
mwamuzi hakuwa na tabu, bali
kifaa alichovaa mkononi
kilimwonesha kwamba ni bao, licha
ya kipa Tito Mannone kuuvuta
mpira haraka kutoka nyuma ya
mstari.
Wakati timu zikielekea kukamilisha
kipindi cha pili huku kocha wa
Chelsea, Jose Mourinho akijidai kwa
kutembea tembea eneo lake la
kujidai, Borini aliwaadhiri dakika ya
88
Walipoingia katika muda wa zaida,
walitoshana nguvu huku kila
upande ukikosa mabao na alikuwa
mchezaji wa Korea, Ki Sung-Yueng
aliyewatesa mabeki, akageuka na
kuweka mpira kimiani dakika ya
118.
MANCHESTER CITY NUSU FAINALI
Manchester City wameingia nusu
fainali ya Kombe la Ligi msimu huu.
Man City wanaofundishwa na
Manuel Pellegrini walivuka baada
ya kupata ushindi wa mabao 3-1
dhidi ya vijana wa Leicester City
wanaocheza kwenye Championship.
Man City wanaojulikana zaidi siku
hizi kwa mtindo wao wa kuachia
mvua ya mabao wakiwa nyumbani,
lakini jioni ya Jumanne hii walikuwa
ugenini.
Kwa hiyo matatu kutoka kwa
Aleksandar Kolarov na Edin Dzeko
aliyefunga mawili, yaliwatosha
wakati wenyeji walipata bao la
kufutia machozi kutoka kwa Lloyd
Dyer.
Jumatano hii katika robo fainali
nyingine, Stoke watakuwa wenyeji
wa Manchester United wakati
Tottenham Hotspur waliomfukuza
kocha wao, Andre Villas-Boas
watakabiliana na West Ham kwenye
dimba lile lile ambalo Liverpool
waliwanyoa 5-0 Jumapili hii.


posted by kulwa ngatigwa

Thursday, 12 December 2013

PICHA: MAHAFALI YA TANO YA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII BUHARE, MUSOMA YALIVYOFANA

gud lukin
picha na kitamonga
wamependeza
wamepoz
niceee
blogger!!! kulwa ngatigwa
poz kwa poz
wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja
bizzman na kubwa la maadu pricila
tabasam tele
namuona KITA MONGA NAE ALIKUWEPO

posted by kulwa ngatigwa

MUONEKANO MPYA WA AGNES MASOGANGE

Pichani juu ni taswira za mpya za Video Queen wa Bongo , Agness Gerald ' Masogange ' alizotupia kupitia ukurasa wake wa Instagram .

posted by kulwa ngatigwa

Wednesday, 11 December 2013

Manji ajitoa Yanga SC

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga , Yusuf Manji.

MWENYEKITI wa Klabu ya
Yanga, Yusuf Manji,
ametangaza rasmi kutowania
tena nafasi ya uenyekiti
kwenye uchaguzi mkuu wa
klabu hiyo utakaotangazwa
baadaye mwakani.
Manji alichukua wadhifa huo
mwaka jana baada ya
kuondolewa kwa aliyekuwa
Mwenyekiti, Lloyd Nchunga,
aliyekuwa amebakiza miaka
miwili ya uongozi wake
klabuni hapo .
Manji ambaye pia ni mfadhili
wa klabu hiyo alitoa tamko juu
ya nia yake hiyo jana kwenye
makao makuu ya klabu hiyo
yaliyopo Jangwani, Kariakoo
jijini Dar es Salaam huku
akitoa sababu kuwa ni
kuwapisha wengine wenye
uwezo wa kuiongoza timu hiyo
nao kuchukua jahazi.
Amesema ametangaza
kutowania nafasi hiyo mapema
ili kuwapa nafasi nzuri
wanaotaka kufanya hivyo
wajipange mapema .
“Sitagombea tena uenyekiti
kwenye uchaguzi ujao,
nitawaachia wengine
waendeleze hapa nilipoishia
mimi , nimetangaza mapema ili
wanaoitaka hii nafasi
wajipange, maana wapo wenye
nia lakini wanahofia kuchuana
na mimi .
“Ninaweza kugombea lakini si
sasa labda baadaye na siyo
uchaguzi huu, nitafikiria
kwanza kabla ya maamuzi
hayo, ” alisema Manji .
Kiongozi huyo aliongeza kuwa
ataendelea kuiongoza Yanga
kwa miezi saba iliyosalia.
Aidha, alisema kuwa bado
tarehe rasmi ya uchaguzi huo
haijafahamika na kudai kuwa
itajulikana mara baada ya
Mkutano Mkuu wa Yanga
utakaofanyika Januari 19 ,
mwakani.
“Nikishajitoa rasmi kwenye
madaraka ya uongozi wa Yanga
baada ya kuwa nimemaliza
muda wangu nitaendelea kuwa
shabiki wa kawaida wa Yanga
kama ilivyo kwa wengine na
kuhusu udhamini litabaki kuwa
suala la klabu kuchagua
mdhamini wao,” alisema
Manji.


posted by kulwa ngatigwa

Tuesday, 10 December 2013

MZEE SMALL YUPO HAI, TAARIFA ZA KIFO CHAKE NI UZUSHI

Mzee Small akiwa na mkewe.

KUNA taarifa zilizagaa kuwa
msanii mkongwe wa
vichekesho na maigizo
nchini, Said Ngamba ‘Mzee
Small’ amefariki dunia.
Taarifa hizo ni za uongo na
uzushi maana mwandishi
wetu ameongea na mke wa
Mzee Small pamoja na Mzee
Small mwenyewe ambaye ni
mzima kabisa ! Mke wa Mzee
Small anadai usiku kucha
hajalala maana alikuwa
anapokea meseji za pole
kutoka kwa watu mbalimbali
kuhusu taarifa hizo za
uzushi. Mzee Small
mwenyewe amesema : "Mimi
ni mzima kabisa japo bado
nasumbuliwa na ugonjwa
wa kiharusi ( stroke )"


posted by kulwa ngatigwa

MANCHESTER UNITED YASABABISHA KIFO KENYA

mwili wa jamaa huyo ukiwa chini

Shabiki wa soka nchini Kenya
ambaye ni fan wa kutupa wa Man
United John Macharia amejiua
wikiendi hii akijirusha kutoka
ghorofa ya saba katika Apartment
anayoishi baada ya timu yake ya
Manchester United kufungwa na
Newcastle siku ya Jumamosi.


posted by kulwa ngatigwa

PICHA: NICKI MINAJ AKISHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO

msanii nicki minaj akisherekea kutimiza miaka 31 leo

posted by kulwa ngatigwa

ALERT: MECHI YA KILI STARZ DHIDI YA KENYA YAHAIRISHWA, SASA KUCHEZWA SAA 12 NA NUSU JIONI

Kili Stars vs Kenya Kombe
la Chalenji: Tumearifiwa muda wa
mechi ya Tanzania VS Kenya sasa ni
SAA 12 NA NUSU,


posted by kulwa ngatigwa

Zitto: Sh2trilioni zinatoroshwa kila mwaka kukwepa kodi

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe

Dodoma. Bunge limeelezwa zaidi
ya Dola za Marekani 1.25 bilioni
sawa na Sh2 trilioni hutoroshwa
na kupelekwa nje ya nchi kila
mwaka kwa lengo la kukwepa
kodi.
Taarifa hiyo imetolewa wakati
wingu zito likiwa limegubika
uwasilishaji wa ripoti ya kikosi
kazi cha Serikali
kilichochunguza sakata la Sh315
bilioni zilizofichwa na
Watanzania katika mabenki
nchini Uswisi.
Takwimu hizo zilitolewa juzi na
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Zitto alisema taarifa mbalimbali
zinaonyesha kuwa Tanzania
inapoteza kila mwaka mapato
hayo ambayo ni sawa na
asilimia tano ya Pato la Taifa
kupitia uhamishaji huo haramu.
“Uhamishaji huu haramu wa
fedha kupelekwa nje ya nchi
hufanywa kwa lengo la kukwepa
kulipa kodi au wahusika
kuepuka kukamatwa na fedha
walizopata kwa kupokea
rushwa,” alisema Zitto.
Kamati hiyo imependekeza
Bunge kutunga sheria
itakayodhibiti uhamishaji
haramu au ufichaji wa fedha nje
ya kwa lengo la kuogopa
kukamatwa na rushwa, kufanya
ufisadi na kukwepa kodi.
Zitto alisema hayo ni moja ya
maazimio yaliyofikiwa katika
mkutano wa 10 wa Jumuiya ya
Kamati za Hesabu za Serikali za
Mabunge (Sadcopac) ya Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(Sadc).
Alisema katika mkutano huo
uliofanyika Septemba 2 hadi 7,
mwaka huu Jijini Arusha,
wajumbe waliazimia
kuhamasisha mabunge ya nchi
zao kutunga sheria kudhibiti
uhamishaji huo wa fedha.
Wiki iliyopita, mbunge wa
Kisesa, Luhaga Mpina (CCM),
alikaririwa akisema bungeni
‘hapatatosha’ kama ripoti ya
mabilioni ya Uswisi
haitawasilishwa katika Bunge
hili.
Mpina alisema yeye ni miongoni
mwa wabunge waliohojiwa
baada ya kutamka bungeni kuwa
zaidi ya Sh11.9 trilioni
zimetoroshwa kutoka Tanzania
kati ya mwaka 1970 na mwaka
2008.
“Nilipolisema hilo jambo
niliikabidhi Serikali kupitia
Bunge taarifa za tafiti
mbalimbali ili ifuatilie. Baadaye
Zitto akaja na hoja ya bilioni
314… tunataka taarifa
hatutanii,” alisema.
Ripoti hiyo ilikuwa iwasilishwe
Bunge la Aprili lakini Serikali
ikaomba muda zaidi na kuahidi
kuiwasilisha katika Mkutano wa
14 wa Bunge unaoendelea Mjini
Dodoma.

chanzo""""mwananchi


posted by kulwa ngatigwa

Jina la JK laongoza marais 100 watakaomzika Mandela

President Jakaya Kikwete

Johannesburg. Serikali ya Afrika
Kusini, imetoa orodha ya majina
ya wakuu wa nchi na Serikali 91
ambao wamethibitisha kushiriki
katika shughuli zinazohusiana
na safari ya mwisho ya Rais wa
kwanza mzalendo wa taifa hilo,
Nelson Mandela.
Jina la Rais Jakaya Kikwete ni la
kwanza katika orodha hiyo
inayowaweka viongozi hao
katika makundi kutokana na
mabara wanakotoka. Rais
Kikwete alitarajiwa kuwasili
jana usiku tayari kuhudhuria
Ibada ya Kitaifa ya Mandela
ambayo imepangwa kufanyika
leo kwenye Uwanja wa FNB
(Soccer City).
Kabla ya Serikali kutoa orodha
hiyo, Waziri wa Uhusiano wa
Kimataifa wa Afrika Kusini,
Maite Nkoana-Mashabane
alisema wakuu wa nchi na
Serikali 53 walikuwa
wamethibitisha lakini jana
mchana idadi hiyo ilikuwa
imeongezeka na kufikia 91.
Kulikuwa na wasiwasi kwamba
huenda idadi hiyo ikaongezeka
na kuzidi 100.
Msemaji wa Wizara ya Uhusiano
wa Kimataifa ya Afrika Kusini,
Clayson Monyela aliwataja
marais wengine kutoka Afrika
kuwa ni kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo (DRC),
Joseph Kabila, Hifikepunye
Pohamba wa Namibia, Mike Sall
wa Senegal, Allessane Ouattara
wa Cote d’Ivoire, Goodluck
Jonathan wa Nigeria, Robert
Mugabe wa Zimbabwe, Dennis
Sassou-Nguesso wa Congo
Brazaville, John Dramani wa
Ghana na Ali Bongo wa Gabon.
Kutoka Amerika ya Kusini ni
marais Nicolus Maduro Moros
wa Venezuela na Dilma Rousseff
wa Brazil ambaye ataambatana
na marais wanne wastaafu wa
nchini kwake.
Waziri Mkuu wa Bahamas, Perry
Christie, Rais wa Guyana, Donad
Ramotar, Rais wa Haiti, Michael
Martelly na Rais wa Jamaica,
Portia Miller, wakati kutoka
Asia, kutakuwa na marais
Pranab Mukherjee wa India na
Hamid Karzai wa Afghanistan.
Rais Francois Hollande wa
Ufaransa, Waziri Mkuu wa
Australia, Tony Abbot, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon
Tayari Rais wa Marekani,
Barrack Obama na mkewe
Michelle walishathibitisha
kushiriki, pia watangulizi wake,
Bill Clinton, George W. Bush na
Jimmy Carter wanatarajiwa
kushiriki katika mazishi ya
Mandela yatakayofanyika Qunu,
Mthatha Jumapili.
Armando Guebuza wa
Msumbiji, , Abdelkader Bensalah
wa Algeria, Makamu wa Rais wa
Angola, Manuel Vicente, Rais wa
Niger, Issoufou Mahamdou,
Kaimu Rais wa Agentina, Amado
Boudou, Waziri Mkuu wa New
Zealand, John Key na Rais wa
Bangladesh, Abdul Hamid MD
Abdul.
Malkia Haakon wa Norway,
Mfalme wa Philippe wa Ubelgiji,
Rais wa Pakistan, Mamnoon
Hussain, Rais wa Benin, Boni
Yayi, Rais wa Palestina
Mahmoud Abbas, Rais wa
Botswana, Seretse Ian Khama,
Rais wa Ureno, Anibal Cavaco
Silva na Mfalme wa Saudi
Arabia, Muqrin bin Abdulaziz
Al-Saud, Rais wa Burundi, Pierre
Nkurunziza, Rais wa Saharawi,
Mohamed Abdelaziz, Waziri
Mkuu wa Canada,
Stephen Harper wa Chad, Idriss
Deby Itno, Rais wa Serbia,
Tomislav Nikolic, Makamu Rais
wa China, Yuanchao, Rais wa
Shelisheli, James Alix Michel,
Rais wa Comores, Dr Ikiliou
Dhoinine na Mfalme wa
Hispania, Felipe de Borbon.
Rais wa Sri Lanka, Mahinda
Rajapaksa, Makamu Rais wa
Sudan, Hassan Salih, Rais wa
Suriname, Desire Delano
Bouterse, Rais wa Slovenia,
Pahor, Rais wa Croatia, Josipovic
Ivo, Rais wa Sudan Kusini, Salva
Kir Mayardit, Rais wa Cuba,
Raul Castro Ruz, Rais wa
Djibouti, Ismail Omar Guelleh,
Waziri Mkuu wa Swaziland, Dr
Sibusiso Dlamini, Waziri Mkuu
wa Ethiopia, Ato Hailemariam
Dessalegn na Rais wa Equatorial
Guinea, Obiang Mbasogo.
chanzo"""mwananchi


posted by kulwa ngatigwa

Kilimanjaro stars kuivaa Harambee stars leo

Timu hiyo ya Kilimanjaro Stars
itacheza saa 7:30 mchana kwenye
uwanja huo ambao katika mchezo
wa kwanza ilicheza hapo na kutoka
sare ya bao 1-1 na Zambia, ambayo
itacheza na Sudan nusu fainali ya
pili mjini Mombasa.
Katika uwanja ambao Stars
itachezea kuna huduma za kifahari
vyumbani kama runinga za kisasa
zilizounganishwa na digitali,
vinywaji laini vya kila aina, chai na
maji ya moto ya kuoga jambo
ambalo linaufanya uwe tofauti na
viwanja vingine vya Afrika
Mashariki na Kati ingawa bado
nyasi haziridhishi hasa mvua
inaponyesha.
Kocha wa Stars, Kim Poulsen
amesisitiza kwamba katika mchezo
huo watashambulia kama
walivyofanya dhidi ya Uganda mjini
Mombasa mwishoni mwa wiki.
Kim alisema: “Ni mchezo mgumu
sana ulioko mbele yetu lakini
naamini kwamba tupo tayari
kushinda katika mazingira yoyote
yale, nina kikosi imara ambacho
kimeimarika kimchezo, nina imani
tutavuka.”
“Hakutakuwa na mabadiliko
makubwa sana kikosini kwa vile
tuna wachezaji wengi ambao wako
tayari kwa mchezo,lengo sasa ni
kucheza fainali na ninaamini huo
uwezo upo tuna mastraika wazuri,
mabeki na viungo.
“Tutacheza mchezo kwa staili
tofauti zaidi, tunajua Kenya itakuwa
na faida ya uenyeji kuanzia
mashabiki na kila kitu lakini
haitatusumbua, tutafanya kazi yetu
uwanjani,”alisisitiza Poulsen
ambaye asilimia kubwa ya kikosi
chake wachezaji wake wamefanya
vizuri kwenye ligi zao.
Habari za ndani zinadai kwamba
Kenya ilifanya mpango wa
kuhamisha mchezo huo kutoka
Mombasa hadi Machakos kutokana
na hali ya hewa.
Mombasa ni joto, hali ambayo
Tanzania wameizoea lakini Kenya
inawapa taabu kutokana na
wachezaji wake kuzoea baridi ya
jijini Nairobi. Kocha Adel Amrouche
alisema; “Tanzania ni ngumu ina
mastraika wazuri, tunajua inaingia
ikiwa na morali ya kumtoa bingwa
mtetezi, lakini sisi tutacheza soka
yetu na ninaamini Kenya kiufundi
ipo sawa tayari kwa fainali za
Alhamisi.”
Kenya itakuwa ikiwategemea
mastraika wake Allan Wanga na
Jacob Kelli huku Stars ikiwa na
ukuta imara wa Kelvin Yondani na
Said Morad huku langoni akizuia
Ivo Mapunda.
Kiungo cha Stars huenda
akasimama Athuman Iddi ‘Chuji’ na
Frank Domayo ambao watakuwa
wakitengeneza mipira kwa
wachezaji wa pembeni Amri Kiemba
na Mrisho Ngassa.
Stars imeonyesha mabadiliko
makubwa kiuchezaji haswa baada
ya kuingia kwa Mbwana Samata na
Thomas Ulimwengu ambao
wameonyesha kujiamini na
wanacheza soka la kufundishwa
jambo ambalo limewafanya wawe
gumzo zaidi.
chanzo. mwanaspoti


posted by kulwa ngatigwa

Monday, 9 December 2013

Kenya yaanza njama kwa Kili Stars

Uganda imeliachia Kombe la Chalenji baada ya kuchapwa kwa penalti 3-2 na Kilimanjaro Stars kwenye Uwanja wa Manispaa ya Mombasa.

Mombasa.Wenyeji Kenya
wameingia mchecheto na makali
ya Kilimanjaro Stars baada ya
kulazimisha mchezo wa nusu
fainali ufanyike Machakos
badala ya Mombasa.
Awali nusu fainali hiyo ilikuwa
ichezwe Mombasa, lakini
kutokana na hali ya joto ambayo
inaibeba Tanzania kulinganisha
na Kenya ambayo wachezaji
wake wengi wanaishi Nairobi
kwenye baridi.
Baada ya mechi dhidi ya
Rwanda, ambapo Kenya
ilishinda bao 1-0, Kocha Adel
Amrouche alikiri kwamba; “Hali
ya hewa ya Mombasa si nzuri
kwetu ni joto kiasi na wachezaji
wangu hawajazoea.”
Habari za ndani zinadai baada
ya Uwanja wa Kisumu
kushindikana kumalizika kwa
wakati waandaji walipanga
mechi za nusu fainali zichezwe
Mombasa na fainali ikachezwe
Nyayo mjini Nairobi, lakini kwa
hali waliyoiona katika mechi za
juzi Jumamosi wenyeji
wakaamua kupeleka mechi ya
Kili Stars dhidi ya Kenya huko
Machakos. Mechi nyingine ya
nusu fainali itachezwa mjini
Mombasa.
Habari za ndani zinadai kwamba
Adel amewaambia viongozi wake
kwamba endapo Kenya ikicheza
na Stars mjini Mombasa itakuwa
kwenye wakati mgumu kutokana
na Tanzania kuzoea hali ya joto
na vilevile ina sapoti kubwa
Mombasa kwa vile ni jirani na
Tanga.
Kenya iko kwenye presha ya
kufuzu fainali kwani siku ya
fainali nchi hiyo itakuwa
ikisherehekea miaka 50 ya
uhuru wake.
UGANDA WAUTEMA UBINGWA
Uganda imeliachia Kombe la
Chalenji baada ya kuchapwa kwa
penalti 3-2 na Kilimanjaro Stars
kwenye Uwanja wa Manispaa ya
Mombasa.
Kocha wa Uganda, Sredejovic
Milutin ‘Micho’ na wachezaji
wake waliingia kwenye mchezo
huo kwa kujiamini, ambapo
walicheza kwa kutulia na
kushambulia kwa kumtumia
winga Dan Sserunkuma
aliyetumia dakika 16 tu kufunga
bao la kuongoza kabla ya Mrisho
Ngassa kusawazisha dakika mbili
baadaye na akafunga tena la pili
dakika ya 38.
Beki mrefu wa Uganda, Martin
Mpunga alifunga bao la pili la
Uganda dakika ya 73 na
kusababisha timu hizo kwenda
kwenye penalti kwani dakika 90
zilimalizika kwa sare ya mabao
2-2.
Stars ilianza kuwachanganya
Uganda mapema baada ya
kusawazisha bao lao na
kuwaongeza jingine na
kuwalazimisha kwenda kipindi
cha kwanza wakiwa nyuma kwa
mabao 2-1.
Hali hiyo ilizua utata kwenye
vyumba vya kubadilishia nguo
kwani kocha Micho alisikika
akiwafokea wachezaji wake na
kuwaambia waache upuuzi kwa
vile wamebeba hadhi ya
mamilioni ya raia wa Uganda.
chanzo-mwananchi


posted by kulwa ngatigwa

MAAJABU 10 MSIBA WA MANDELA

Kifo chake kimeushtua
ulimwengu na kwa mara ya
kwanza katika historia, dunia
nzima imesimama nyuma ya
jemedari huyo , kila mmoja
akionesha masikitiko yake .
Wakati dunia ikisubiri mazishi
yake ambayo pia yatavunja
rekodi ya mazishi yote
yaliyowahi kufanywa tokea
kuumbwa kwa uso wa dunia
hapo Desemba 15 mwaka huu,
Uwazi limebaini maajabu kumi
yanayoambatana na msiba
huo.
AIR FORCE ONE KUBEBA
MARAIS WATANO WA
MAREKANI
AIR Force One ni ndege
inayombeba Rais wa Marekani
aliye madarakani na
kumpeleka popote duniani .
Lakini katika hali ya
kushangaza, Idara ya Usalama
ya Marekani imetoa ruhusa
kwa marais wastaafu wakiwa
na wake zao , kuandamana na
Rais Barak Obama kuhudhuria
mazishi ya shujaa huyo wa
dunia.
Hii ni mara ya kwanza katika
historia ya taifa hilo lenye
nguvu kubwa duniani
kuwapakia katika ndege hiyo
yenye kila kitu ndani yake,
marais wake kwa wakati
mmoja .
Marais hao ni Obama
mwenyewe na mkewe
Michelle, George Bush na
mkewe Laura, Bill Clinton na
mkewe Hillary , Rais wa 39 wa
Marekani, Jimmy Carter naye
atakuwepo ila baba yake
George W. Bush , George Bush
senior huenda asiende
kutokana na urefu wa safari
hiyo.
QUNU; KIJIJI
KITAKACHOLNDWA KULIKO
VYOTE DUNIANI
Mandela alizaliwa katika Kijiji
cha Qunu, kilichopo katika
Jimbo la Eastern Cape ,
kilometa 32 Kusini Magharibi
mwa mji wa Mthatha .
Kutokana na tukio hilo kubwa
la mazishi, Jeshi la Afrika
Kusini ambalo ni bora zaidi
barani Afrika, limechukua
jukumu la kusimamia ulinzi
wote. Lakini uwepo wa Rais
Obama na watangulizi wake
wanne, utaifanya nchi hiyo
kuchukua tahadhari zaidi ya
kuhakikisha hakuna dosari
yoyote ya kiusalama
inayoweza kujitokeza .
Ulinzi huo umeimarishwa zaidi
kutokana na ukweli kwamba
viongozi wakubwa karibu wote
wa dunia watahudhuria
mazishi hayo , akiwemo Papa
Francisco, Waziri Mkuu wa
Uingereza, David Cameron na
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon. Hakuna
uwezekano wowote wa Al
shaabab kusababisha rabsha
kwani wameshadhibitiwa kwa
ulinzi mkali.
MANDELA ALIKUWA ‘GAIDI ’
PEKEE ALIYEGEUKA KUWA
SHUJAA
Kwa miaka mingi, mataifa ya
magharibi pamoja na Marekani
walimchukulia Mandela na
harakati zake kama gaidi .
Wakati wa utawala wa ubaguzi
wa rangi nchini Afrika Kusini,
chama cha ANC kilikuwa na
jeshi lake lililofahamika kama
Umkhonto we Sizwe. Wazungu
wa Magharibi na Marekani
ambao walikuwa wakiwaunga
mkono Makaburu , waliiona
ANC kama kikundi cha kigaidi
na hivyo Mandela naye
akawekwa katika orodha ya
magaidi duniani .
Hata hivyo, baada ya kutoka
jela na kuchaguliwa kuwa Rais
wa Afrika Kusini , Mandela
aligeuka kuwa kipenzi cha
watu hao ambao walilazimika
kumuondoa katika orodha ya
magaidi na leo hii akiwa
amefariki dunia , anapewa
heshima kubwa kuliko
aliyowahi kupewa mzungu
yeyote duniani.
MWEUSI PEKEE
ALIYENYENYEKEWA NA
WAZUNGU
Hayati Mandela ndiye mtu
mweusi pekee duniani
aliyewahi kupewa heshima
zisizo na mfano tokea
kuumbwa kwa dunia. Mara
baada ya kutangazwa kwa kifo
chake, viongozi wa mataifa
yote makubwa duniani
walionesha masikitiko yao na
kila mmoja alimsifu kama mtu
wa aina ya pekee kuwahi
kuwepo chini ya jua (ukiachia
mbali mitume na manabii) .
JENGO LA SERIKALI NEW
YORK LAPAKWA RANGI YA
BENDERA YA SAUZI
Jengo moja la serikali jijini
New York , Marekani
limebadilishwa taa za
kulipamba na kuonesha
bendera ya taifa la Afrika
Kusini.
WENYEJI WAHAMA , WAGENI
WAMILIKI NYUMBA QUNU
Kijiji cha Qunu, sehemu
ambayo yatafanyika mazishi ya
Mandela, kuna eneo dogo
kulingana na ugeni mkubwa
unaotarajiwa kuwepo . Taarifa
kutoka huko zinasema wenyeji,
pamoja na machungu
waliyonayo kutokana na kifo
cha mzee huyo , pia
watafaidika kiuchumi kutokana
na wageni wengi kutaka
kupata nyumba za kukaa
wakati wakiendelea na
maombolezo.
Wanaotafuta nyumba kijijini
hapo ni pamoja na watu
kutoka vyombo mbalimbali
vya habari , mashirika ya
kimataifa na wageni binafsi .
Inadaiwa kuwa wenyeji
wanasogea katika vijiji vya
jirani ili kupangisha nyumba
zao kwa muda.
MECHI ZA LIGI KUU
ENGLAND ZAANZA KWA
SALA
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida, Chama cha Soka cha
England ( FA) kiliamuru mechi
zote za ligi kuu zilizochezwa
wiki iliyopita , lazima zianze
kwa sala maalum ya kumuenzi
mzee Mandela .
Hii ni mara ya kwanza kwa
agizo hilo kutolewa kwa
heshima ya kiongozi mstaafu
aliyefariki dunia asiye
Mwingereza, tena akitokea
barani Afrika. Tukio kama hilo
pia limefanywa na Shirikisho
la Soka la Kimataifa ( FIFA)
ambalo limeamuru bendera
yake iliyo katika mataifa yote
wanachama duniani, ishushwe
nusu mlingoti kwa heshima ya
Tata Madiba !
NASA YATOA ZAWADI YA
PICHA YA SAUZI KUTOKA
ANGANI
Taasisi ya utafiti wa anga za
juu nchini Marekani (NASA)
kwa kutambua mchango
mkubwa wa Mandela katika
amani ya dunia, imetangaza
kutoa zawadi kwa watu wa
Afrika Kusini , itakayoonesha
picha ya nchi hiyo
inavyoonekana kutoka angani .
UINGEREZA YAAGIZA BALOZI
ZOTE KUSHUSHA NUSU
MLINGOTI
Serikali ya Uingereza
imeziagiza balozi zote za kigeni
zilizopo nchini humo kushusha
bendera zao nusu mlingoti
kama moja ya heshima na
maombolezo ya kifo cha Mzee
Nelson Mandela .
Hili ni agizo la aina yake
kuwahi kutolewa kuhusiana na
msiba wa kiongozi yeyote,
kwani suala la kushusha
bendera mara nyingi ni
uamuzi wa serikali husika na si
kwa shinikizo kama ilivyotokea
Uingereza.
AMSAFIRISHA PAPA
MAZISHINI
Historia ya utumishi wa
kiongozi mkuu wa Madhehebu
ya Romani , papa haioneshi
kama aliwahi kuhudhuria
mazishi ya rais au rais
mstaafu, kitendo cha Papa
Francisco kuhudhuria mazishi
hayo kumeongeza ajabu katika
mazishi ya Mandela , wengi
wakisema hakina hakuwa mtu
wa kawaida.

PICHA= POLISI JAMII CUP, DODOMA


Posted via Blogaway