Wednesday, 15 January 2014

DIVA ATIMULIWA CLOUDS FM!!!

WATANGAZAJI maarufu Bongo wa
Redio Clouds Fm ya jijini Dar es
Salaam, Hamis Mandi ‘B 12’, Adam
Mchomvu na Loveness Malinzi ‘Diva’,
wamepigwa chini na kituo hicho,
Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Habari za chini kwa chini kutoka kwa
chanzo chetu zinasema kuwa uongozi
wa Clouds umefikia hatua hiyo
baada ya kuchoshwa na tabia ya
utovu wa nidhamu wa watangazaji
hao.
Hata hivyo, madai ya mitaani
yanasema kwamba watangazaji hao
wamepigwa chini kwa kosa la
kukacha sherehe za maadhimisho ya
miaka 14 ya Clouds FM,yaliyofanyika
hivi karibuni katika Viwanja vya
Mwembeyanga, Temeke, Dar.
Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji
wa Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba na kumwuliza juu ya ishu
hiyo ambapo alikiri.
“Ni kweli tumefikia uamuzi wa
kuwasimamisha B 12, Diva na
Mchomvu baada ya kukiuka baadhi
ya makubaliano baina yao na ofisi
hivyo kusababisha usumbufu
mkubwa ambao ulitulazimu kuingia
gharama ambazo hazikutarajiwa.
“Hatutakuwa nao kwa muda
usiojulikana ingawa watu wengi
wamekuwa wakinihoji juu ya hilo
lakini watachotakiwa kuelewa ni
kwamba hakuna ofisi isiyokuwa na
sheria na taratibu za kuongoza watu
wake, sasa hao wamevunja taratibu
zetu,” alisema Ruge bila kufafanua
zaidi.
Alipoulizwa ni taratibu zipi
watangazaji hao walizovunja alisema:
“Nashindwa kueleza kosa la kila
mmoja ila naomba nieleweke kuwa
hao watangazaji kwa sasa
tumewasimamisha kwa muda
usiojulikana wakati tukifikiria cha
kufanya. Muhimu hapo ni kwamba
wamekwenda kinyume na
tulivyokubaliana.”


Posted via Blogaway

No comments:

Post a Comment