MSANII aliyefanya poa kwenye
filamu kadhaa ikiweko ya Malaika,
Devotha Julius Mbaga ‘The First
Born’ yuko katika wakati mgumu
kufuatia kunasa ujauzito ambao
kwa sasa siyo siri tena.
Akizungumza na mwandishi wetu
hivi karibuni, mmoja wa rafiki wa
msanii huyo (jina kapuni) alisema
kuwa licha ya msanii huyo kufanya
siri juu ya ujauzito huo, lakini kwa
sasa dalili zinaonesha kuwepo kwa
ujauzito na kwamba kwa sasa
anatumia muda mwingi kuwa
nyumbani ili kukwepa macho ya
wengi kugundua juu ya kubugia
kwake ‘kijusi’.
“Kwa sasa Devotha ana mimba,
lakini anafanya siri kubwa sana ili
watu wengi wasijue (wakiwemo
waandishi), ndiyo maana haonekani
mara kwa mara, anatumia muda
mwingi kuwa nyumbani,” kilisema
chanzo hicho.
Devotha alipoulizwa kuhusu ishu
hiyo, amekiri kuwa na kitumbo cha
miezi minne.
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment