Fani ya urembo imekua kivutio
sana kwa watu wengi hapa bongo,
moja ya matamasha yaliyona
watazamaji wengi pindi mda wake
unapofika ni tamasha la Miss
Tanzania. Mashindano haya
yamekua kivutio sana kwani tofauti
na kuwashindanisha warembo
mbalimbali pia hua kunakuwepo na
burudani mbalimbali kama ngoma
za asili, burudani kutoka kwa
wasanii mbalimbali wa bongoflava
n.k
But watu wengi hawajui historia ya
mashindano hayo, wapi yalipoanzia
hadi hivi sasa yamekua na wapenzi
wengi. Leo admin wenu wa
Bongoclan katika pitapita zangu
nkakutana na picha ya washindi wa
tatu wa mashindano ya kwanza
kabisa ya kumtafuta miss zanzibar.
Mashindano hayo yalifanyika
mwaka 1968. Hakika ukiitizama
picha hii bado ina ubora hii
inamaanisha kua mtunzaji wake
alikua makini sana kuilinda picha
hii. Kama unavyoona katika picha
hapo juu mshindi wa kwanza
alikua mrembo Bedive Khamis,
mshindi wa pili alikua mwanadada
Hanifa ibrahim na aliyeshika nafasi
ya tatu alikua Doreen D'souza.
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment