STAA wa sinema Bongo, Aunt
Ezekiel amejikuta akizichapa na
mwanamke aitwaye Sarah
Mwakapala ambaye miaka mitano
iliyopita waliwahi kugombea penzi
la mwanaume anayejulikana kwa
jina la Mwilu Mwilola ‘Silva’.
Tukio la ugomvi huo lilichukuwa
nafasi juzi katika Ukumbi wa Letasi
Lounge uliopo Victoria jijini Dar
ambapo kulikuwa na sherehe ya
kuzaliwa ya rafiki yao
aliyetambulika kwa jina la Jamila.
Ilielezwa kuwa, wakati sherehe
ikiendelea, Sarah alisimama na
kwenda mahali alipokaa Aunt na
kuanza kumfanyia fujo huku wageni
waalikwa wakishind
wa kujua chanzo.Chanzo
kilichoshuhudia sekeseke hilo
kilibainisha kuwa, Aunt alionekana
kujishusha akimwomba Sarah
kuacha mambo ya ugomvi, lakini
Sarah hakukubali ndipo mtiti
ulipozidi kuwa mkubwa na
kusababisha wavuane mawigi yao
yaliyokuwa yamewapendeza.
“Ghafla tulishangaa Sarah anainuka
na kwenda kumvamia mwenzake
pasipo kujua nini chanzo. Sijui
wenyewe bado wana mabifu yale ya
kipindi kile au vipi!” kilisema
chanzo hicho.
Hata hivyo, mdau maarufu wa
mastaa wa Kibongo, Nice Chande
ambaye alikuwa karibu na Aunt,
aliingilia ugomvi huo na kutuliza
hali ya hewa kwa kumdhibiti Sarah.
“Unajua kuna watu hawajifunzi kwa
wenzao kuhusiana na vifo vya siku
hizi, we unakuja kumfanyia fujo
mwenzako, mnapigana bila sababu
yoyote. Je, ghafla mwenzio siku
zake za kuishi kumbe zimeisha
unapata kesi la ajabu, unaanza
kujilaumu,” alisema Nice.
Baada ya hali ya hewa kutulia,
paparazi wetu alimfuata Sarah
kutaka kujua kulikoni amuanzishie
fujo mwenzake, hakuweza kujibu
chochote huku akiingia kwenye gari
na kukimbilia Kituo cha Polisi
Oysterbay kufungua kesi.
Taarifa zilizopatikana baadaye
wakati gazeti hili linakwenda
mitamboni zinadai kuwa, Aunt
naye alikimbilia polisi na kukuta
Sarah ameshafungua malalamiko
lakini waliyamaliza palepale kituoni
na msala ukaishia hapo.
Posted via Blogaway
No comments:
Post a Comment