Nyerere: Kama vile nakufananisha?
Mandela: Hata mimi naona sio sura
ngeni?
Nyerere: We ndie Mandela eee?!
Mandela: Ndiyo mimi haswa miaka
14 ni mingi.
Nyerere: Sana!!.
Mandela: Sasa nitakaa wapi mbona
hakueleweki huku?
Nyerere: We ngoja utapaelewa tu.
Nyerere: Eeh!! vipi huko Tanzania?
ulitembelea hata hivi karibuni?
Mandela:
Eeeh! we acha tu, huko mara Zitto
msaliti, mara Umeme mgawo miezi
sita, mara mgomo wa Gesi haitoki
Mtwara, mara kifo cha Mwangosi,
mara Dawa za Kulevya, mara Meno
ya Tembo, mara kuchoma
Makanisa, mara mabomu kwenye
mikutano ya hadhara na
makanisani, mara Ufisadi, mara
Dr. Ulimboka na Kibanda
kung’olewa kucha na meno kwa
plauzi, mara Division 5, mara
Udini, mara ngumi Bungeni, mara
kifo cha Dr Mvungi, mara tindikali
kwa mapadri, mashehe na wageni,
mara Kagame kuishambulia
Tanznia, Petroli kuchakachuliwa,
mara wengine wanasema eti
Muungano ulioasisi unatokana na
Visiwa vya Zimbabwe na Zanzibar
na sio Tanganyika tena, mara
muungano wa serikali tatu ndio
unaotakiwa, mara Kigamboni
kapewa Obama, mara Bushi na mke
wake kaja Tanzania, Clinton na mke
wake kaja Tanzania, Kamerun na
mke wake kaja Tanzania, Xiing wa
uchina kaja Tanzania, mara puttin
wa Urusi kaja Tanzania. Yaani
hekaya ni ndefu bora urudi
ukayashuhudie mwenyewe.
Mara Mandeal alipomrushia macho
swahiba wake kumbe kashazimia
saa nyingi
Posted via Blogaway