Friday, 27 June 2014

RAIS KENYATTA BINGWA KWA TWITTER BARANI AFRIKA, AMPIKU KAGAME



Rais Kenyatta amempiku Paul Kagame wa Rwanda kwa idadi ya wafuasi kwenye Twitter.
Rais wa Kenya uhuru Kenyatta ndiye Rais anayejishughulisha zaidi kwenye mtandao wa Twitter barani Afrika.
Kenyatta amempiku Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Kenyatta ambaye amekuwa mamlakani tu kwa mwaka mmoja, amejipatia wafuasi 456,209, yuko mbele ya mwenzake wa Rwanda Paul Kagame mwenye wafuasi 408,353 ambaye amekuwa mamlakani tangu mwaka 2000, miaka sita kabla hata ya Twitter kuanzishwa.
Rais wa Afrika Kusini anayesifika kwa kashfa mbali mbali, Jacob Zuma ana wafuasi 325,896 akishikilia nafasi ya tatu.
Hata hivyo swali ni je maerais hawa hutumia vipi Twitter? Je wao huwa na mazungumzo ya moja kwa moja na wafuasi wao?
Waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi '@AmamaMbabazi,' ndiye kiongozi mwenye kuwasiliana zaidi na wafuasi wake duniani kwenye Twitter huku akiwajibu maswali yao kwake.


408,353, idadi ya wafuasi wa Rais Kagame kwenye Twitter
Asilimia tisini na tano ya mawasiliano yake kwenye Twitter ni '@replies,' ishara ya kuwajibu wafuasi wake. Utafiti huu ni kwa mujibu wa utafiti wa kimataifa kuhusu viongozi wanavyojishughulisha na Twitter, wenye mada, Twiplomacy.
Waziri mkuu mpya wa India, Narendra Modi ana wafuasi milioni 4,967,847 , na anaelekea kushinda Ikulu ya white House ambayo ina wafuasi milioni 4,976,734 katika nafasi ya tano.
Zaidi ya asilimia 83 ya mataifa yote duniani yana uwakilishi katika Twitter, na asilimia 68 ya viongozi wana akaunti za twitter kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Burson-Marsteller, nchini Marekani.
Viongozi wanaofuatwa sana kwenye Tiwtter ni pamoja na Barack Obama (@BarackObama) akiwa na wafuasi milioni 43, Papa Francis (@Pontifex) ana wafuasi milioni 14 akifuatiwa na Rais wa Indonesia Susilo Bambang Yudhoyono (@SBYudhoyono) akiwa na wafuasi milioni tano.


Jacob Zuma kama rais anashikilia nafasi ya tatu kwa idadi kubwa ya wafuasi wa Twitter Afrika.
Rais Barack Obama alikuwa kiongozi wa kwanza kuanzisha akaunti ya Twitter mwaka 2007.
Kati ya serikali 643 zenye akaunti za Twitter ambazo zilitathminiwa katika nchi 161, ni mataifa 32 pekee hasa yaliyo Afrika na Asia ya Pacific ambayo hayana shughuli nyingi kwenye Twitter.
Utafiti huo pia ulifichua kuwa mawaziri wa mataifa ya kigeni hutumia sana Twitter kutafuta ushirikiano wa kidiplomasia.
BBC

KISA VIBINTI CHINI YA MIAKA 18, MZEE WA KANISA AAIBIKA!, ABAMNWA LIVE GUEST


Stori: Richard Bukos na Issa Mnally Tumekwisha! Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za Kibongo, Debora Jacob, Ijumaa lina kisanga cha aina yake.
Mzee wa kanisa la kiroho aliyetajwa kwa jina la Luca Pesa,
HABARI KAMILI
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka 18.

Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
TUHUMA NZITO
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, ikiwa kwenye mingo zake, ilipokea simu kutoka kwa dada aliyejitambulisha kwa jina moja la Diana na kujieleza kuwa anatoka kundi la sanaa za maigizo la Vivif lililopo Segerea jijini Dar.

OFM: Ndiyo hujakosea unazungumza na
OFM, tukusaidie nini?
Diana: Kuna mzee wa kanisa la kiroho la (anataja jina la kanisa hilo) lililopo maeneo ya Segerea, aliomba kuwa mfadhili wa kundi letu.

Akiwa kwenye geti la kanisa.
Tulimkubalia na baada ya muda alianza kutumia fedha zake vibaya kwa kufanya vitendo visivyofaa.
OFM: Vitendo gani visivyofaa?
Diana: Anawarubuni mabinti wadogo anawaweka kambini na kula nao tunda tamtam eti ndiyo tiketi ya kuchezeshwa kwenye maigizo.
OFM: Tiririka!

Diana: Yaani hadi muda huu ninapozungumza na ninyi mzee huyo wa kanisa anachati na msanii mwingine wa kundi hilo. Anaitwa Debora anataka waende kwenye gesti fulani wakanogeshane, wahini tayari mtego umewekwa utafyatuka muda wowote.
UDHALILISHWAJI?
Diana alisema baada ya Debora kuombwa ‘mambo’ ndipo akawataarifu wasanii wenzake na kuwataka wote kwa pamoja waungane kuikomesha tabia hiyo chafu ya Luca anayelichafua kanisa la kiroho na kulidhalilisha kundi lao la sanaa.

OFM MZIGONI
Baada ya kuseti kila kitu, Diana aliiomba OFM iambatane nao kwani muda huo tayari Debora alishatangulia kwenye gesti hiyo kumfuata mzee huyo wa kanisa ambaye alishachukua chumba.

.....akitaitiwa.
Taarifa hiyo ilipokelewa kwa mikono miwili na kiongozi wa OFM ambaye aliwaagiza vijana wake makini ambao walisitisha kazi nyingine za kiintelijensia kisha kuelekeza nguvu zao eneo la tukio.
Vijana hao walitumia pikipiki zao ziendazo kasi ambapo baada ya muda usiozidi dakika ishirini walikuwa wamefika kwenye gesti hiyo.

ENEO LA TUKIO
OFM walipofika eneo la tukio, walikuta kundi la wasanii hao wakimchomoa gesti mzee huyo wa kanisa ambaye aliruka ukuta na kudondokea kwenye matuta ya viazi.

Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo, zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.

Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
KABANG!
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.

APELEKWA MSOBEMSOBE KANISANI
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.

Mtuhumiwa akitembezwa mtaani.
MTAANI WERAAA!
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.

Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
BREKI YA KWANZA POLISI
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO, KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.

Hadi OFM wanaanua jamvi kituoni hapo kanisa lilikuwa likihaha kumchomoa kwa dhamana akisubiri sheria kuchukua mkondo wake.

Tuesday, 3 June 2014

Picha za mitego za Irene Uwoyaa

Gal on fire she is back again staa irene
uwoya, she was quite for a while, lakini
ujio wake mpya alokuja nao umekuwa
wa kishindo n people were so suprised,
kiukweli to staaz kuvaa taulo na kupiga
picha akivaa taulo na kutupia kwenye
mitandao ya kijamii ni jambo la
kawaida sana, leo mtandao wa
makubwa haya tumezinyaka picha hizi
kwenye mitandao ya jamii, na funs
wakawa wanacoment, kuna wengine
walicoment kawaida wengine
waliponda, but all in all kwa mastaa
kama irene uwoya kuvaa taulo
haunikama ni ki2 cha ajabu coz
everybody do so. Alisikika akimalizia
kisema hvyo kwa funs wake


posted by kulwa ngatigwa☆★

Saturday, 25 January 2014

KIPOFU HUYU AMETISHA SAAANA

Kipofu kampiga mtu mpaka
kamuua, akafikishwa
mahakamani;
HAKIMU: Kwanini umefanya
ukatili namna hii
KIPOFU: Mheshimiwa
marehemu alisema
mwenyewe,'Ukinipiga utaona',
kwa vile nilikuwa na hamu
kubwa ya kuweza kuona,
nikajitahidi kumpiga sana ILI
nipone, bahati mbaya kafariki.


Posted via Blogaway